Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
member photo
BALOZI PROFESA ELIZABETH KIAGO KIONDO
Mwenyekiti wa Bodi

Barua pepe:

Simu:

Wasifu

WASIFU WA BALOZI PROF. ELIZABETH KIAGO KIONDO

1. TAARIFA BINAFSI

Jina Kamili: Balozi Profesa Elizabeth Kiago Kiondo

Nchi: Tanzania

Fani: Elimu, Uongozi, Diplomasia na Mitaala

2. ELIMU

Prof. Elizabeth Kiago Kiondo ni mwanataaluma aliyepata mafunzo yake katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM. 

Amesoma mpaka ngazi ya Shahada ya Uzamivu - PhD katika fani ya Elimu.

Pia ana Shahada ya Uzamili na Shahada ya Kwanza katika Elimu na Uongozi.

Ni mtaalamu mahiri katika maeneo ya Maendeleo ya Mitaala, Sera za Elimu, na Uongozi wa Taasisi za Elimu ya Juu.

3. UZOEFU WA KAZI NA HUDUMA

Prof. Elizabeth Kiago Kiondo alianza kazi yake kama Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - UDSM, Chuo cha Elimu.

Katika kipindi chake UDSM, alikuwa miongoni mwa wahadhiri waliotoa mchango mkubwa katika kufundisha, kutafiti na kuboresha mitaala ya elimu ya juu nchini.Baada ya kuhudumu kitaaluma, aliteuliwa na Serikali ya Tanzania kuwa Balozi. 

Katika nafasi hiyo amewakilisha nchi yetu katika ngazi za kimataifa, akidumisha na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kitamaduni na kitaaluma kati ya Tanzania na nchi nyingine.

4. MCHANGO KWA TAIFA 

Sekta ya Elimu: Ameshiriki katika uundaji na ukaguzi wa sera na mitaala ya elimu nchini. Alichangia katika kuimarisha ubora wa walimu na viongozi wa elimu.Uwezeshaji wa Wanawake: Ni kielelezo na kimbilio kwa wanawake wengi waliopo na wanaotaka kuingia katika nyadhifa za uongozi, kitaaluma na diplomasia. Kwa weledi na uadilifu wake, ameisaidia Tanzania kujulikana na kuheshimika kimataifa.

 

HITIMISHO

Balozi Prof. Elizabeth Kiago Kiondo ni miongoni mwa watanzania waliotupa heshima kubwa kupitia elimu, uongozi na diplomasia. Mchango wake unaendelea kuwa chachu kwa vizazi vijavyo.

slot gacor