MKUTANO WA WADAU KWA UHAKIKI WA MTAALA SLADS
24 Apr, 2025
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka na Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea, leo tarehe 11 Machi, 2025 amefungua Mkutano wa Wadau kwa kuhakiki Mtaala wa Chuo cha SLADS.
Katika hotuba yake, Dkt. Ruzegea amewataka washiriki wa Mkutano huo kusikiliza kwa makini wasilisho la Mtaala huo na kujadili namna bora itakayosaidia kumwezesha mwanafunzi kuwa na ujuzi, kuwa Mjasiriamali na mtunza kumbukumbu na takwimu (data).vilevile, amewataka kuhakikisha wanajadili namna bora ya Mtaala utakavyomfanya mwanafunzi na Jamii kwa ujumla kujenga utamaduni wa kujisomea (Reading Culture).
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa Baraza, Kaimu Mkuu wa chuo cha SLADS Bi. Bertha Mwaihojo alieleza kuwa dhumuni la Mkutano huo ni kuwashirikisha Wadau ili kwa pamoja wahakiki Mtaala na kupata mawazo, ushauri na maboresho zaidi kwenye Mtaala huo.
Aidha, Washiriki wa Mkutano walipata wasaa wa kusikilisha wasilisho la Mtaala kutoka kwa Mratibu wa masuala ya Taaluma MkufunzCharles Auckley, kushiriki majadiliano kisha kutoa mapendekezo juu ya uboreshaji wa Mtaala wakiongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Bi. Bertha Mwaihojo na Dkt. Mahija Waziri kutoka NACTVET.
Mkutano wa Wadau kwa uhakiki wa Mtaala umefanyika Chuoni SLADS Bagamoyo, Mkoani Pwani na umewakutanisha Wadau wa Elimu kutoka taasisi za NACTVET na ADEM, Viongozi Wastaafu wa SLADS, Uongozi wa SLADS na Wakufunzi wa SLADS, Watumishi TLSB, Wahitimu wa SLADS (Alumnae) na Viongozi wa Serikali ya Chuo hicho (SLADSSO).