Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
PROF. MKENDA ATETA NA KAMATI YA KITAIFA YA TUZO ZA TAIFA YA UANDISHI BUNIFU YA MWALIMU JULIUS K. NYERERE
24 Apr, 2025
service image
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amefanya kikao na Kamati ya Kitaifa ya Tuzo za Taifa ya Uandishi bunifu ya Mwalimu Julius K. Nyerere, katika Ukumbi wa Mikutano wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) jijini Dar es Salaam, hii leo tarehe 18 Septemba, 2024. Akizungumza katika kikao hicho, Prof. Mkenda amesema kuwa, lengo la kukutana kwao ni kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo suala la uboreshaji wa Tuzo za Mwl. Nyerere za Uandishi bunifu zinazotarajiwa kufanyika Mwezi Aprili, 2025. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kamati ya Tuzo hizo Prof. Penina Mlama, amesema kuwa kwa sasa zoezi la maandalizi ya kupokea miswaada mbalimbali ya Waandishi bunifu linaendelea. Kwa upande mwingine, Katibu Mtendaji wa Baraza za Mitihani Tanzanaia Dkt. Said Mohamed, ametoa Wasilisho la namna mfumo wa Elimu ya Jumla na Amali utakavyotekelezwa nchini. Kikao kati ya Prof. Mkenda na Kamati ya Kitaifa ya Tuzo za Taifa za Uandishi bunifu za Mwalimu Julius K. Nyerere, kimehudhuriwa pia na Viongozi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwemo Naibu Katibu Mkuu Dkt. Charles Mahera, Kamishna wa Elimu Prof. Lyabwene Mtahabwa na Wakuu wa taasisi kutoka TET, NACTVET, NACTE, VETA, Kamati ya Kitaifa ya Tuzo na TLSB ambapo Mkurugenzi Mkuu Dkt. Mboni Ruzegea amehudhuria.