Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
SLADS NA ADEM WAKUTANA
24 Apr, 2025
service image
Kaimu Mkuu wa chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) Bi. Bertha Mwaihojo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Maulid J. Maulid, wamefanya kikao maalum na kujadili mpango mkakati wa kufanya mafunzo na kubadilishana uzoefu baina ya taasisi hizo mbili. Hayo yamejiri tarehe 24 Januari, 2025 katika ofisi za chuo cha SLADS zilizoko eneo la Ukuni Bagamoyo, mkoani Pwani. Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na njia bora ya kutoa mafunzo na kuwanoa Wakufunzi/Wakutubi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa uweledi na ufanisi. Aidha, kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba TLSB Dkt. Rehema Ndumbaro.