Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
KIKAO KAZI CHA WENYEVITI NA WAKUU WA TAASISI ZA UMMA - 2025
25 Aug, 2025
service image
Pichani: Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TLSB, Prof. Rwekaza S. Mukandala (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TLSB, Dkt. Mboni A. Ruzegea (Kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja tarehe 24 Agosti, 2025 katika ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEO's FORUM 2025). Kikao kazi hicho kinafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) jijini Arusha, kinaratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na hufanyika kila mwaka kujadili mafanikio, changamoto na mustakabali wa mashirika ya umma nchini. Mada Kuu ya Kikao Kazi hicho kwa mwaka huu 2025 ni 'Ushirikiano Endelevu wa Kibiashara katika Mazingira Shindani Kimataifa - Nafasi ya Mashirika ya Umma'. Aidha, kikao kazi hicho kimeanza tarehe 23 Agosti 2025 na kitatamatika tarehe 26 Agosti, 2025.