Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
WANAWAKE WA TLSB WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
08 Mar, 2026
service image
Watumishi Wanawake wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, Maktaba za mkoa wa Dar es Salaam wamehudhuria Viwanja vya Mburahati Barafu, yalipofanyika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kimkoa, leo tarehe 8 Machi, 2025 jijini Dar es Salaam. Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe.Albert Chalamila, ambaye ameitaka jamii hususan wanawake kuachana na mikopo umiza na isiyo ya lazima na badala yake wakope kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi. Aidha, Chalamila ameiasa jamii kuwajali na kuwalinda wazazi wao hasa akina mama, akisisitiza kuwa mwanamke ni nguzo muhimu ya familia, jamii na taifa kwa ujumla. Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa kitaifa na kimataifa tarehe 8 Machi kila mwaka, yakilenga kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya jamii pamoja na kuhamasisha usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake yenye kauli mbiu, ”Haki na Usawa kwa Wananwake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050”.