Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
TLSB YAFANYA MAFUNZO YA VVU, UKIMWI, RUSHWA NA AFYA YA AKILI KWA WATUMISHI SLADS
24 Apr, 2025
service image
Bodi ya Huduma za Maktaba Tanazania (TLSB), imefanya Semina kuhusu VVU, Ukimwi, Rushwa na Afya ya Akili kwa Watumishi wa SLADS ili kuwaongezea uelewa, maarifa na njia za kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza katika mazingira yao ya kazi. Semina hiyo imefanyika tarehe 24 Januari, 2025 katika ukumbi wa Mikutano SLADS Bagamoyo, Mkoani Pwani. Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba TLSB Dkt. Rehema Ndumbaro (akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu), ameishukuru Idara ya Rasilimali watu na Utawala TLSB kwa kuaandaa Semina hiyo kwa Watumishi wa SLADS kama ilivyokua kwa Watumishi wa TLSB na kuwashukuru Wawezeshaji kwa kuitikia wito wa kutoa mada katika Semina hiyo. Vilevile, aliwataka Watumishi SLADS kusikiliza kwa umakini mada zote na kushiriki zoezi la hiyari la upimaji lililofanyika baada ya mafunzo hayo. Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa, TLSB inaunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa elimu juu ya masuala ya VVU, Ukimwi, Magonjwa yasiyoambukiza, Rushwa na Afya ya akili. Hivyo, katika kuunga mkono juhudi hizo, Bodi imekua ikitenga bajeti kila mwaka ili kuwezesha Semina hizo kutolewa kwa Watumishi. Miongoni mwa Mada zilizowasilishwa katika Semina hiyo ni; Elimu kuhusu VVU, Ukimwi na Magonjwa yasiyoambukiza kutoka kwa Mwezeshaji Dkt. Zena Kimanga kutoka TACAIDS/Hospitali ya Bagamoyo, Elimu ya Rushwa na athari zake kwa Watumishi wa Umma iliyotolewa na Wakili Mary Mwakatobe Afisa kutoka TAKUKURU Wilaya ya Bagamoyo na Afya ya Akili kutoka kwa Mwezeshaji Dr. Secilia kutoka Hospitali ya Bagamoyo Mkoani Pwani. Pichani: Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma za Maktaba Dkt. Rehema Ndumbaro akifungua mafunzo hayo, sambamba na picha za matukio mbalimbali katika semina hiyo tarehe 24 Januari, 2025 katika Ukumbi wa Mikutano SLADS Bagamoyo, Mkoani Pwani.