Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
TLSB YATOA ZAWADI KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM SHULE YA MSINGI UHURU MCHANGANYIKO DAR ES SALAAM
28 Apr, 2025
service image
Watumishi wanawake wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) Makao Makuu Dar es salaam, tarehe 7 Machi, 2024 wametembelea shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko iliyoko jijini Dar es Salaam na kuwapatia zawadi wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TLSB, Mwenyekiti wa wanawake TLSB Bi. Paulina Mwangwa, amesema wamerudisha kwa jamii matendo ya huruma kwa kuwapatia zawadi watoto na wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma shuleni hapo. Bi.Paulina ameongeza kuwa, TLSB inaendesha Maktaba maalum kwa wanafunzi wasioona katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, hatua inayopelekea wanafunzi hao kupata vitabu vya rejea wakiwa shuleni hapo. Akipokea zawadi hizo, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo Bi. Hajrat Kashakara amewashukuru wanawake wa TLSB kwa kuwakumbuka watoto hao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Katika ziara hiyo, Wanawake TLSB Dar es Salaam wamepeleka zawadi zifuatazo; pipi, biscuit, sharubati, sabuni za kufulia nguo na dawa za meno ambazo watoto wanatumia.