Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
TLSB YAWAHAMASISHA WAANDISHI WACHANGA KUJISAJILI
28 Apr, 2025
service image
TLSB kupitia Kitengo chake cha Bibliografia ya Taifa (NBA) kimepokea nakala za vitabu kwa ajili ya kuweka namba tambuzi kutoka kutoka kwa Mwandishi mchanga Peter Nsangano aliyeandika kitabu kiitwacho JICHO LA FURSA ili kuwafikia wasomaji walioko nchini na nje ya nchi. Akipokea nakala za Kitabu hicho, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Bibliografia ya Taifa (NBA) Bi. Irene Moshi, ameeleza miongoni mwa majukumu ya Kitengo cha NBA ni kutoa mwongozo wa namna ya uandishi, kupokea machapisho na kuhifadhi yakiwa katika mfumo wa kielekroniki pamoja na nakala ngumu sambamba na kuhakiki kilichomo katika nakala kama yamekidhi vigezo vyote vya maadili ya kimaudhui, pamoja na kusajili na kutoa namba tambuzi. Aidha, ametoa rai kwa waandishi wote nchini kufika NBA na kujisajili kwa lengo la kupata namba tambuzi kwa  kila kazi ya uandishi yaani  ISBN kwa Vitabu na ISSN kwa Majarida na Magazeti inayoweza kulinda maslahi ya mwandishi mwenyewe. Bi Irene ameongeza kuwa, hasara zitokanazo na waandishi kutojisajili katika mfumo wa Maktaba ni pamoja na kupoteza idadi kubwa wa wasomaji wanaotembelea maktaba pamoja kukosa hati ya miliki inayopelekea kukosa mapato ya machapisho hayo. Kwa upande wake mwandishi wa kitabu cha JICHO LA FURSA ndug. Peter Msongano, ameushukuru Uongozi wa TLSB kwa huduma nzuri na elimu kuhusu Maktaba katika  kuhakikisha usalama wa kisheria wa Maandiko na Machapisho kwa kizazi cha leo na vizazi vijavyo. Aidha, ameongeza kuwa, JICHO LA FURSA ni kitabu chake cha kwanza ambacho kimeeleza fursa mbalimbali zinazotokana na matumizi sahihi ya Teknolojia kwa kupata soko kwa urahisi, Fursa zinazotokana na jiografia ya sehemu husika sambamba na elimu katika kuleta maendeleo katika jamii.