Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
UDAHILI WA MASOMO SLADS - MUHULA WA SEPTEMBA, 2024
27 Mar, 2024
service image
  Chuo Cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka- (SLADS) ni Chuo cha Serikali kinachoendeshwa na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Chuo kina usajili wa kudumu wa Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTEVET) kwa namba REG/PWF/006. Mkuu wa Chuo anakaribisha maombi ya mafunzo ya Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka muhula mpya wa masomo utakaoanza Septemba 2024/2025 kwa ngazi zifuatazo:-   1. Cheti cha awali cha Utunzaji Kumbukumbu (Basic Technician        Certificate in   Records and Archives Management) NTA Level 4. 2. Cheti cha awali cha Ukutubi (Basic Technician Certificate in Library and Information Management) NTA Level 4. 3. Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu (Technician Certificate in Records and Archives Management) NTA Level 5 4. Cheti cha Ukutubi (Technician in Library and Information Management) NTA Level 5 5. Stashahada ya Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu (Ordinary Diploma in Library, Records and Information Studies) NTA level 6.   SIFA ZA KUJIUNGA 1. Kwa ngazi ya Cheti cha awali (NTA Level 4) muombaji awe amehitimu elimu ya kidato cha nne (4) na kupata alama nne (4) za ufaulu wa D au zaidi (Four passes). 2. Kwa ngazi ya NTA Level 5 muombaji awe na cheti cha Form 6 mwenye ufaulu wa Principal pass 1 na subsidiary pass 1 au ufaulu wa cheti cha awali Cha NTA Level 4 Records and Archives Management au NTA Level 4 Library and Information Management.   JINSI YA KUOMBA  Tuma maombi kwa njia ya mtandao (online application) kupitia www. slads.ac.tz.   Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Chuo: www. slads.ac.tz  barua pepe : slads@tlsb.go.tz/aumanagement@slads.ac.tz   AU PIGA SIMU   Namba:     0766 - 220405            0652 – 001692               0753 – 643020            0654 - 399565               0718 - 432102