Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
UZINDUZI MA MAKTABA YA JAMII MACOBICA - MBINGA, RUVUMA
31 Dec, 2025
service image
Jamii imetakiwa kutumia Maktaba kujifunza, kujielimisha, kujiongezea maarifa na ubunifu ili kuwa na jamii iliyoelimika na kufikia lengo la Dira 2050. Hayo yamesemwa tarehe 2 Desemba 2025 na Naibu Katibu Mkuu (Elimu), wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mgeni Rasmi Dkt. Hussein Mohamed Omar wakati akizindua Maktaba ya Jamii MACOBICA  (Maguu Community Based Information Centre Association) iliyopo Maguu, Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma. Dkt. Omar amesema kuwa, Maktaba inajukumu la kutoa huduma zake bila ubaguzi wa rangi wala rika sawasawa na Sera ya Elimu nchini. "Maktaba zinatakiwa ziwe na programu kwa ajili ya rika zote, ili kila mtu katika jamii aweze kupata programu kulingana na mahitaji yake, hii itaharakisha kupatikana kwa jamii iliyoelimika sawasawa na dhamira ya Dira 2050 kuwa na jamii iliyoelimika" amesema Dkt. Omar. Awali Akimkaribisha Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TLSB Dkt. Wakuru Manini, amepongeza uongozi wa Maktaba ya Jamii MACOBICA kwa kuja na wazo zuri la kuanzisha Maktaba hiyo, ambayo itakua kitovu cha Maarifa na Ujuzi kijijini Maguu. Naye Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea, amesema kuwa TLSB imepeleka vitabu vyenye maudhui ya ndani vilivyonunuliwa kwa fedha kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania zaidi ya Milioni 10, vilevile, kupaka rangi jengo la maktaba na kununua rafu za vitabu (book shelves) ikiwa ni juhudi za kupeleka huduma za Maktaba kwa jamii ambapo amesema maktaba hiyo itakua chuo cha wazi kwa watu wote kujipatia maarifa na ujuzi. Kwa upande mwingine, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Ndumbaro ameushukuru uongozi wa TLSB kwa kuungana na MACOBICA kusogeza hiduma za maktaba kijijini Maguu na kuahidi kuhamasisha jamii kutumia Maktaba hiyo. Naye Mwenyekiti wa Maktaba ya Jamii MACOBICA ndug. Simon Mahai, amesema lengo la kuanzishwa kwa maktaba hiyo lilikua ni kusaidia wanafunzi hasa wanapomaliza darasa la saba, wapate sehemu ya kujiongezea maarifa badala ya kuzurura mtaani na kujiingiza kwenye makundi yasiyo sahihi na kufanya vitendo vya kihalifu.