Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
WATUMISHI WA TLSB WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MAHITAJI YA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU
28 Apr, 2025
service image
Watumishi wa TLSB, TBA,TGFA, DCEA na TIC wamepatiwa mafunzo kuhusu Mahitaji ya Rasilimali Watu Serikalini, tarehe 07 Desemba 2023, katika Ukumbi wa Mikutano TLSB Makao Makuu Dar es Salaam. Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TLSB Dkt. Mboni Ruzegea ametoa rai kwa watumishi hao kuzingatia mafunzo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendelezaji Taasisi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndug. Nolasco Kipanda amesema kuwa, serikali imeanzisha mifumo mbalimbali ili kurahisisha utendaji kazi na muda. Kipanda ameongeza kuwa, kwasasa Watumishi wa Umma hawana haja ya kuhangaika na makaratasi kwa Maafisa Rasilimali watu na Utawala katika kufatilia mikopo, bali huomba mikopo hiyo moja kwa moja kupitia mifumo wakiwa ofisini. Mafunzo hayo yametolewa na Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ndug. Waziri Mkumbo.