Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
MAFUNZO YA UANDISHI BUNIFU KUIBUA VIPAJI KWA WASIOONA
15 Oct, 2026
service image
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Mh. Balozi Prof. Elizabeth Kiago, leo tarehe 15 Oktoba 2026, amefungua mafunzo ya uandishi bunifu wa hadithi za watoto kwa watu wenye mahitaji maalumu, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Maktaba Kuu ya Taifa, jijini Dar es Salaam. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafnzo hayo, Prof. Kiago amesisitiza umuhimu wa kuibua na kukuza vipaji vya uandishi kwa makundi yote na hasa ya wenye mahitaji maalum, amesema kuwa katika ulimwengu wa sasa unaotegemea taarifa na maarifa, hakuna mtu anayepaswa kuachwa nyuma. Pia amehimiza kufanyika kwa tafiti ili kubaini iwapo kazi za waandishi zinawafikia walengwa na kusomwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili na utamaduni wa Mtanzania ili kazi hizo ziweze kudumu na kuenziwa na vizazi vijavyo. Kwa upande wake, Bw. Mwamwingila Goima, mwandishi na mtunzi wa kazi za fasihi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mtalimbo Publishers, amesema mafunzo hayo kwa waandishi wasioona yanalenga kuwawezesha washiriki kuandika na kusimulia hadithi zao wenyewe, badala ya kutegemea watu wengine kuwaandikia simulizi zao. Aidha, Bw. Goima amesema kuwa wakati Kiswahili kikiendelea kupata nafasi katika jukwaa la kimataifa, ni muhimu Watanzania wenye mahitaji maalumu, wakiwemo watu wasioona, kupewa fursa na ujuzi wa kuandika vitabu ili vipaji vyao na simulizi.  

slot gacor