Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
WAZIRI MKENDA ATAKA MAFUNZO YA UKUTUBI YAENDANE NA TEKNOLOJIA
09 Oct, 2026
service image
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alitembelea Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka Bagamoyo (SLADS), mkoani Pwani, Oktoba 5, 2026, na kujionea mazingira na miundombinu ya chuo. Katika ziara hiyo, alisisitiza kuboresha mafunzo ili yaendane na maendeleo ya teknolojia na mahitaji ya soko la ajira. Aliagiza kufanya utafiti kwa kuwashirikisha wahitimu na wataalamu wa sekta husika ili kubaini maeneo yanayohitaji maboresho, hususan katika zama za kidijitali. Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Dkt. Mboni Ruzegea, alisema Serikali imetenga shilingi milioni 572 kwa ajili ya kuboresha majengo na vifaa katika taasisi zilizo chini ya Bodi hiyo. Pia alieleza mipango ya kupanua miundombinu ya SLADS ili kuimarisha mafunzo na kuongeza udahili.

slot gacor