Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
WAZIRI MKENDA KUZINDUA MFUMO JUMUISHI WA MAKTABA MTANDAO WA TAIFA
17 Oct, 2026
service image
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, anatarajiwa kuzindua Mfumo Jumuishi wa Maktaba Mtandao wa Taifa (INDLS), katika Kongamano la Nne la Kitaifa la Huduma za Maktaba litakalofanyika Oktoba 20 hadi 22 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Dkt. Mboni Ruzegea, amesema hayo leo tarehe 17 Oktoba, 2026 katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya Taifa ya kuwa, uzinduzi wa mfumo huo ni hatua muhimu katika mageuzi ya huduma za maktaba nchini, kwa kuwa unalenga kurahisisha upatikanaji wa taarifa, rasilimali za maktaba na maarifa kupitia teknolojia ya kidijitali.  Amesema mfumo huo unatarajiwa kupanua fursa za wananchi kupata huduma za maktaba, huku ukiimarisha ujifunzaji na matumizi ya maarifa kwa maendeleo ya jamii.   Vilevile amesema kongamano hilo litajadili maboresho ya sera na mwongozo wa usimamizi wa huduma za maktaba, maendeleo ya wataalamu wa maktaba na namna ya kuimarisha huduma hizo ili ziendane na mahitaji ya wananchi.  Pia kutakua na Tamasha la Vitabu na Usomaji pamoja na Soko la Mashirikiano litakalowakutanisha TLSB na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuboresha huduma za maktaba nchini.  Kongamano hilo lenye na kaulimbiu isemayo, “Maboresho ya Huduma za Maktaba Kupitia Mageuzi ya Kidijitali, Kukuza Maarifa na Ujuzi kwa Maendeleo Endelevu”. 

slot gacor