Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
SLADS ALUMNI WAKUTANA, WAAHIDI KUENDELEZA CHUO CHAO
25 Nov, 2026
service image
Wahitimu wa Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka (SLADS) wamekutana leo, tarehe 25 Novemba 2026, katika viwanja vya chuo hicho Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, kujadili namna ya kuimarisha umoja wao na kuchangia maendeleo ya chuo. Mkutano huo umehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa TLSB na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Dkt. Mboni Ruzegea, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi. Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Ruzegea amesisitiza SLADS kuendelea kuwa kitovu cha mafunzo bora ya Ukutubi kwa kuzingatia dhana ya “Training for Quality and Competence.” Amepongeza umoja wa Alumni wenye wanachama 776, akieleza umuhimu wake katika kuwainua, kuhamasisha na kuwapa wengine fursa, huku akiwashukuru kwa michango yao ya hali na mali katika maendeleo ya chuo. Aidha, ameeleza kuwa chuo kinatambua na kuthamini wahitimu wa SLADS ambao majina yao huenda hayasikiki sana, lakini wanafanya mambo makubwa na yenye mchango muhimu katika jamii. Ameongeza kuwa chuo kimeanza kufanya Tracer Study kwa wahitimu wake ili kufuatilia maendeleo yao, kutambua mafanikio yao na kujua mchango wao katika jamii na sekta mbalimbali. Alumni Prof. Ali Mcharazo na Dkt. Juliana Manyerere wamehimiza umoja huo kuwa daraja la kulea, kuwapa fursa na kuwatambulisha wahitimu katika jamii, huku Prof. Mcharazo akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi na wakutubi ili kuimarisha uwezo wa tafiti na mchango wa SLADS katika maendeleo ya kitaifa kupitia Sera ya TEHAMA. Mkutano huo pia umejadili historia, mwelekeo, matarajio na changamoto za chuo, ikiwemo uhaba wa vifaa vya TEHAMA, zilizowasilishwa na Kaimu Mkuu wa Chuo, Bi. Bertha Mwaihojo. Aidha, Kaimu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Bi. Flora Joseph, amewahimiza Alumni kujiunga na umoja huo na kuchangia maendeleo ya chuo. Mkutano umehitimishwa kwa kupitisha Katiba ya Umoja wa SLADS Alumni iliyowasilishwa na Ndugu Leonard Ngowo, pamoja na uchaguzi wa viongozi wa umoja huo.

slot gacor