Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania

TLSB Logo TLSB Logo
Tafuta kwenye kwa
VITABU VYA UTALII NA KAMUSI ZA LUGHA TANO ZAZINDULIWA
17 Oct, 2026
service image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Ndg. Methusela Ntonda, amezindua vitabu vya utalii na kamusi za lugha za Kifaransa, Kiingereza, Kijapani, Kiitaliano na Kiswahili katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Vitabu Tanzania, Dar es Salaam, Oktoba 16, 2026. Akizungumza katika uzinduzi huo, Ntonda amesisitiza ushirikiano katika uzalishaji wa machapisho bora na kukuza utamaduni wa kusoma. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB), Dkt. Mboni Ruzegea, amewahimiza waandishi na wachapishaji kuwasilisha machapisho maktaba kwa ajili ya kuhifadhiwa na ..upatikanaji wa namba za Utambulisho wa Vitabu (ISBN). Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wachapishaji wa Vitabu Tanzania (PATA), Bw. Hermes Salla, amesisitiza umuhimu wa Sera ya Taifa ya Kusoma na Kuandika, huku Dkt. Jossam Mungure, Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), akieleza kuwa vitabu hivyo vinalenga kuitangaza Tanzania kimataifa. Vitabu vya utalii vimechapishwa na Mbiu na Elite, huku kamusi zikichapishwa na APE Network kwa uwezeshaji wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa (TACAF).

slot gacor